Ilala yawaka moto, DC Mjema atangaza kiama cha majambazi


Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema watapiga kambi katika mitaa yote ya Vingunguti kwa ajili ya kufanya operesheni nyumba hadi nyumba ili kudhibiti tatizo la vibaka wanaopora watu hususani akina mama.

DC Mjema ameyasema hayo katika mkutano wa wananchi  wakati akijibu malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi na kuwataka kuorodhesha majina ya watuhumiwa wanaojihusisha na vitendo hivyo ikiwemo changamoto ya vibaka na ujambazi vinavyowakosesha usingizi katika maeneo yao ili hatua zichukuliwe.

Awali wananchi hao walielezea kero mbalimbali ikiwemo wafanyabiahara katika eneo la Machinjio ambao wametakiwa kuhama bila kupatiwa eneo mbadala ukosefu wa mitaro mitaani usafiri na changamoto kubwa ya maji iliyoongoza kulalamikiwa na wananchi wengi katika mkutano huo.