Mahakama yamuachia huru Baba Levo


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Crayton Chipando maarufu kwa jina la Baba Levo ameachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kigoma leo  Jumatano, Septemba 19, 2018.

Baba Levo alikuwa akikabiliwa na mashtaka matatu ya kushambulia, kufanya vurugu na kutoa lugha ya matusi dhidi ya muuguzi Christina Gervas wa Zahanati ya Msufini.