Mkuu wa Mkoa was Dar es Salaam Paul Makonda amekagua miradi ya Ujenzi wa barabara Wilaya ya Kigamboni na kutoa maelekezo kwa Tanrods kuweka alama kwenye maeneo yote yaliyokatwa au waliochimba ili kuweza kusaidia kupunguza ajali hasa kwa waendesha Bodaboda.
Rc Makonda ameyasema hayo leo alipofanya ziara katika Manispaa hiyo, na kukagua kazi inayofanywa na Tanrods pamoja na Tarura na kuwapongeza kwa kazi wanayoifanya ndani ya Manispaa hiyo.
Amesema watahakikisha katika barabara zinazojengwa katika Daraja la Nyerere, Kigamboni wanaweka miundombinu mizuri ili kuwafanya wananchi wanaozungukwa na barabara hizo kunufaika na mradi huo wa barabara.
"Katika barabara sita zianzojengwa katika Daraja la Kigamboni nimemwambia Mkuu wa Wilaya kuhakikisha tunajenga miundombinu rafiki kwa wananchi wanaozungukwa hapa, ikiwemo kujenga Stand, kuhakikisha kuna sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu na mferji wa mita 400 ambao umeshatengenezwa na kuhakikisha maji yanapita"Amesema Makonda.
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano pale wanapohitajika hasa wanapoitwa katika mikutano ili kushiriki katika kutatua kero zinazokabili Wilaya hiyo.
Amesema katika halmashauri ya Kigamboni kunajengwa shoorom ya kisasa ya Afrika Mashariki, hivyo wameamua kutatua kero za miundombinu ikiwemo barabara umeme Pamoja na maji ili kusaidia kuwepo kwa Viwanda vitakavyoongeza pato la Manispaa hiyo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara. Amemshukuru Rc Makonda kwa kufanya ziara Katika halmashauri yake, na kutoa maelekezo katika miradi ya kimkakati
Hasa kwenye miradi ya barabara.

