Waamuzi watakaochezesha mechi ya Stars na Cape Verde watajwa


Shirikisho Ia Mpira wa Miguu Barani Africa CAF Iimetaja waamuzi kutoka nchini Mali kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 kati ya Cape Verde na Tanzania 'Taifa Stars' katika Uwanja wa Estadio National 12 Oktoba, 2018.

Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Boubou Traore akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Drissa Kamory Niabe, Mwamuzi msaidizi namha 2 Baba Yomboliba na Mwamuzi wa akiba Gaoussou Kane na Kamishna wa Mchezo anatokea G. Equatorial Tadeo Nsue Onva.

Aidha mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa Oktoba 16, 2018 Kwenye Uwanja wa Taifa wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Djibouti

Mwamuzi wa katikati atakuwa Soulelman Ahmed Djama, na Mwamuzi msaidizi namba 1 Farhan Bogoreh Salime, Mwamuzi msaidizi namba 2 Rachid Waiss Bouraleh na Mwamuzi wa akiba Bilal Abdallah Ismael.

Kamishna wa mchezo anatokea Malawi Maxwell Mtonga, Mtathmini waamuzi anatokea Rwanda Michael Gasingwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items