Serikali yashusha neema kwa wakulima Zanzibar


Na.Thabit Madai, Zanzibar
Wakulima 52 kutoka Unguja na Pemba wamepatiwa mafunzo ya kulinda pamoja na kuhifadhi mimea na mazao kwa maradhi na wadudu waharibifu ili kuendeleza kilimo chao na kuwa na tija kwa Taifa.

Mafunzo hayo ya siku 30 yametolewa na Serikali ya watu wa China chini ya kituo cha tafiti za kilimo nchini humo cha chinnes academy of tropical agriculture  science pamoja na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya kilimo, Maliasili,Ufugaji na Uvuvi Pamoja na  Chuo cha kilimo na tafiti kizimbai,  Zanzibar.

Akifunga mafunzo hayo ya siku 30 Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili Ufugaji na Uvuvi Dk Makame Ali Ussi aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kuyatumia kwa kuwaelimisha wakulima wenzao ili kuondokana na kero ya muda mrefu ya  maradhi na wadudu sugu wanaoharibu mimea na mazao .

Alisema pindi watakapoyatumia vizuri mafunzo hayo yatawawezesha kuongeza uzalishaji mkubwa wa mazao pamoja na kuongeza kipato chao binafsi na kuchangia kukuza uchumi wa  Nchi kupitia sekta ya kilimo.

“Mafunzo haya mlioyapata yana tija kubwa katika sekta kilimo ambapo mkiyaendeleza hakika tutapata faida kubwa katika maendeleo ya Zanzibar” Alisema Naibu Waziri wa kilimo.

Alisema wizara itachukua jukumu la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wakulima waliopatiwa mafunzo hayo ili kuona kwa namna gani mafunzo hayo yamewafaidisha na kuwa chachu yamaendeleo kwa Zanzibar.

Nae Mkurugenzi wa kituo cha Tafiti ya Sayansi ya kilimo nchini Lin Kuiran alisema lengo la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu na  kuwaongezea ujuzi wakulima wa Zanzibar kwa namna ya kulinda mazao kwa njia mabadala bila ya kutumia kemikali.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items