Wadau waombwa kuunga mkono sekta ya Afya


Na.Thabit madai, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka wadau mbali mbali wa maendeleo kuwaunga mkono kwa kuwasaidia vifaa ambavyo vitasaidia kuwezesha kutoa huduma bora katika sekta ya afya.

Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Afya zanzibar Harusi Saidi Suleiman mara baada ya kupokea Vifaa-tiba kutoka Shirika la kuhudumia Watoto UNICEF (Zanzibar).

Alisema ni vyema kwa mashirika binafsi kuuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha kuduma bora kwa wagonjwa ili wananchi wa kipato cha chini waweze kunufaika na huduma za matibabu zinazotolewa katika Hosptali na Vituo cha afya.

Aidha alisema  mpaka sasa wizara ya afya imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito pamoja na kununua vifaa-tiba.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema  watahakikisha wanatumia vyema vifaa walivyokabidhiwa  ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kuwataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu ili kuimarisha huduma za matibabu.

Awali akikabidhi Vifaa hivyo kwa Wizara ya Afya Mwakilishi kutoka Shirika la kuhudumia Watoto UNICEF Maryam Seif Hemed alisema wataendelea kuunga mkono serikali katika kuwasaidia kina mama na watoto ili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items