https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mtatiro amtaja Lipumba kama sababu ya kuhama CUF, 'Sijanunuliwa' | Muungwana BLOG

Mtatiro amtaja Lipumba kama sababu ya kuhama CUF, 'Sijanunuliwa'


Aliyekua Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro  amefunguka namna alivyohama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi huku pia akimtupia lawama Mwenyekiti wa chama hicho anayetambulika na Msajili, Profesa Ibrahim Lipumba.

Mtatiro amesema hakuna ukweli wowote wa yeye kununuliwa na CCM na kwamba hakuwasiliana na kiongozi yoyote wa chama hicho kuhusu kuomba kujiunga nacho au kuahidiwa nafasi yoyote ya kiuongozi.

" Huwezi kusema kila mtu amenunuliwa lazima ujue kiongozi aliyehama ni nini, vyama vya upinzani wasiishie kupiga kelele kuwa watu wananunuliwa wafanye utafiti kujua kwanini watu wao wanaondoka, wasipojitathimini watajikuta wanapoteza watu wote.

" Hata mimi nilipokuwa Kiongozi nilikua napiga kelele kuwa watu wananunuliwa lakini kwa upande wangu niseme wazi hakuna fedha yoyote ambayo inaweza kuninunua," amesema Mtatiro.

Aidha amesema sababu kuu iliyomfanya kuondoka CUF ni namna ambavyo Lipumba amekuwa akikivuruga chama hicho na kwamba hakua tayari kufanya kazi nae huku akisema amekuwa aking'ang'ania madaraka ya uenyekiti wa chama hicho.