Takribani wagonjwa 700 kwa mwaka hupokelewa katika hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa na matatizo ya ngozi yanayotokana na kumeza vidonge vinavyobadili rangi ya mwili pamoja na vipodozi vyenye kemikali.
Hayo yamesemwa na Dk.Faustine Ndugulile Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto wakati akijibu swali la msingi la Fatma Hassan Toufiq mbunge wa viti maalum.
Ndugulile amesema kuwa watu hao wanaotumia vipodozi hivyo wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya saratani na magonjwa ya ngozi.
Kuhusu kubandika kucha na kope bandia Ndugulile amesema kwa mujibu wa sheria ya chakula dawa na vipodozi sura 219 inayosimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa haitambui suala la kucha za kubandikwa na kope na hivyo serikali haina takwimu ya ukubwa wa tatizo hilo.
