Mabasi saba yanayofanya safari kwenda mikoani yamezuiwa kuendelea na safari mapema leo katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo Jjini Dar es Salaam baada ya kubainika kuwa na hitilafu.
Kutokana na hitilafu hizo wamiliki wa mabasi hayo wametakiwa kuwarudishia nauli abiria ama kuwatafutia usafiri mwingine ili kuendelea na safari zao.
Hatua hiyo imefikia baada ya ukaguzi uliofanywa na kikosi cha usalama barabarani kikiongozwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Abdi Isango, ambapo pia magari yaliobainika na hitilafu ndogo ndogo walitakiwa kurekebisha na kuendelea na safari.