Mambo haya ni muhimu kuyazinagatia wakati unajiandaa na mitihani yako


Benson Chonya
Habari za muda huu mpenzi msomaji wa blog hii ya Muungwana blog bila shaka u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Noamba nichukue walau dakika chache kuweza kukukumbusha jambo hili la muhimu hasa pale unapokuwa unajiandaa kufanya mitihani.

Awali ya yote unatakiwa kufahamu au kujua maeneo ambayo ni muhimu ili uweze kuweka nguvu kubwa katika eneo hilo.

Hili pia ni jambo la msingi kujua wapi unatakiwa kuweka nguvu katika kipindi cha mwisho cha kujiandaa na mitihani yako ya mwisho ,katika kuweka nguvu unatakiwa kuweka mkazo katika mambo makuu  mawili kama ifuatavyo:

Yale masomo ambayo una uhakika unayajua vizuri na uelewa mkubwa.
Mara nyingi kila mwanafunzi anakuwa na masomo ambayo anajua anafanya vizuri hivyo basi ni vizuri kuweka nguvu kubwa katika hayo masomo maana ndio yatanyanyua Division yako ,hakikisha masomo ambayo una uwezo nayo wa kufaulu hukosi chini ya B+ .

Hakikisha unawekeza muda wako katika masomo hayo, unapaswa kujua hayo ndio yanweza kukukomboa lakini kumbuka pia unatakiwa kuweka nguvu pia kwenye masomo mengine maana usije pata A huku kwingine unapata F jua utashusha division yako maana matokeo yote huwa yanatafutwa kwa kwa kanuni ya 'LAW OF AVERAGE'

Uliko na mapungufu ndio kuna alama nyingi
Lakini pia lazima uweke nguvu kubwa kwenye sehemu yenye mapungufu ambayo unajua maswali yake yana maksi nyingi. Kipindi hichi cha mwisho lazima ujue ni eneo gani una mapungufu lakini ni eneo gani pia ambalo linaulizwa sana kwenye mitihani ,hapa sasa ndio umuhimu wa kujua mfumo wa mtihani unavyokuja. Ukishajua mapungufu uliyonayo na wewe mwenyewe huwezi basi mtafute mwalimu au mwanafunzi mwenye uwezo nalo akupe msaada.

Hivyo unapaswa kuyazingatia haya ili uweze kufanya vyema katika maandalizi ya mitihani yako.

Mpya zaidi Nzee zaidi