Msanii Roma alizwa na matapeli wa kimtandao

Rapa Roma amelizwa na matapeli wa mtandaoni.

Hii ni baada ya namba yake ya simu kudukuliwa na kuanza kutumika ndivyo sivyo kwenye mtandao wa WhatsApp. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Roma ameandika;

"Technology ina faida lakini inatugharimu sana, imezuka tabia mtu ana hack number yako ya simu kisha anafungua Whatssap Group na inakuwa inaonyesha kuwa wewe  ndio umefungua hilo group na wewe ndio mmiliki, hii imenikuta mimi na imewakuta wengi," ameeleza Roma.

Kwa sasa Roma anafanya vizuri na wimbo uitwao Kaolewa wa kundi la Rostan (Roma & Stamina)

Mpya zaidi Nzee zaidi