Rais Magufuli awapokea mabalozi wawili, aahidi ushirikiano zaidi


Rais Dk John Magufuli amepokea hati za utambulisho wa mabalozi wawili ambao wameteuliwa kuziwakilisha nchi za Japana na Georgia hapa nchini.

Mabalozi waliokabidhi hati za utambulisho ni Shinichi Goto ambaye ni Balozi wa Japan hapa nchini na Zurab Dvalishivli wa Georgia mwenye makazi yake mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Pamoja na kupokea hati hizo za utambulisho Rais Magufuli amesema Tanzania itaendeleza ushirikianona kukuza uhusiano wake na nchi hizo hasa katika uwekezaj, biashara, ujenzi na miundombinu.

Rais Magufuli amemueleza Balozi wa Japan, Shinichi kuwa Tanzania na Japan zimeshirikiana katika utekelezaji wa miradi mingi ya ujenzi na miundombinu na utoaji wa huduma za kijamii na kwamba anaamini ushirikiano huo utaendelezwa zaidi kwa kuhakikisha miradi inayoendelea inakwenda vizuri na miradi mipya inaongezeka.

Pia Rais Magufuli amemueleza Balozi wa Georgia, Zurab kuwa anatambua yeye ni Balozi wa kwanza kuteuliwa kuiwakilisha nchi hiyo hapa nchini, hivyo amemuomba awalete wawekezaji hasa wa viwanda kutoka Georgia kuja kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji huo.

Mabalozi hao wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Tanzania ili kuendeleza na kukuza uhusiano baina yao.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items