Na.Ahmad Mmow, Kikwa
WANANCHI wa Kijiji cha Kandawale, wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi wamemkataa mtendaji wa kijiji chao kwatuhuma za kukwamisha miradi na matumizi mabaya ya mapato ya kijiji.
Hayo yalijiri jana wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai aliyekwenda katika kijiji cha Mtumbei Mpopela kwa lengo la kusikiliza na wananchi wa kitongoji cha Nangorombe kilichopo katika kijiji cha Mtumbei Mpopela.
Wananchi hao walisema hawamtaki mtendaji huyo kwasababu anakwamisha na kuharibu miradi ya kijiji.Ikiwemo mradi wa trekta ambalo limeharibika,na ubadhirifu wa fedha za kijiji.Hivyo wananchi hao walimuomba mkuu huyo wawilaya baada ya kumaliza kuzungumza nao hakikishe anaondoka nae.Hata hivyo mtendaji huyo hakuwepo kwenye mkutano.
Walisema hata taarifa aliyosomewa na kupewa mkuu huyo wa wilaya ilikuwa imejaa uongo natakwimu za kupikwa.Kwasababu mambo yaliyoelezwa kwenye taarifa hiyo ambayo ilisomwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kandawale kwa niaba ya mtendaji huyo ilificha ukweli na kujazwa uongo. Hasa eneo la kiasi cha fedha zilizotumika,zilizopo na taslimu.
Walisema hadi sasa trekta ambayo ilitolewa na halmashauri ya wilaya kupitia idara yake ya kilimo imeharibika na haifanyi kazi kwa muda mrefu.Huku suala la matengenezo likiwa nisawa na kitendawili.Japokuwa dhamira ya halmashauri nikuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao ya kilimo.
"Mkuu wa wilaya ukisikia watu wanamlalamikia mtu kiasi hicho ujue kunajambo hapo.Usipuuze,chukua,tafakari na ufanye uamuzi.Haiwezekani watu wote wamchukie,"aliongeza kusema Mzee Mtwiku ambae alisisitiza maelezo ya wenzake wengi waliomtuhumu mtendaji.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya,Ngubiagai alisema kwakuzingatia utawala bora hawezi kumchulia hatua bila kujiridhisha juu ya tuhuma hizo.Japokuwa hata yeye alikubaliana na wananchi hao kuhusu walakini uliokuwepo kwenye taarifa aliyosomewa.Kwasababu inamkanganyiko uliowazi ambao hata mtu asiye nataaluma ya uhasibu asingeikubali.
Ngubiagai alisema kufuatia mkanganyiko wa taarifa na maelezo ya wananchi hao atamuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo amtume mkaguzi wa halmashauri hiyo akakague taarifa ya mapato na matumizi ya fedha na mali za kijij hicho.
Kuhusu kadhia ya trekta,Ngubiagai alisema uharibifu wa matrekta haupo katika kijiji hicho tu.Kwasababu takribani vijiji vyote vilivyopewa matrekta na mashine za kusaga zimeharibika.Huku kukiwa hakuna juhudi zilizofanyika nakutoa matokeo chanya yakuzifanyia matengenezo.
"Niliagiza ufanyike ufuatiliaji ili kubaini sababu.Lakini hakuna kilichofanyika na trekata nyingi bado ni mbovu wakati hata ile asilimia ishirini ya fedha za manunuzi ya trekata vijiji hivyo vilitakiwa kulipa,hazijalipwa na vijiji vingi kama sio vyote vilivyopata trekta,"alisema Ngubiagai.
Kuhusiana na hilo mkuu huyo wa wilaya aliwaambia wananchi hao kwamba atamuguaza mkurugenzi mtendaji wa wilaya ahakikishe mkuu wake wa idara ya kilimo anampeleka kwake(mkuu wa wilaya) taarifa itayoeleza trekta zinazofanya mzima,zilizoharibika,sababu za kuharibika na kwanini hazijatengenezwa kwa takribani miaka miwili.Huku akitoa wiki tatu tu baada ya kutoa agizo hilo taarifa hiyo iwe imefikishwa mezani pake.
Alionya kuwa hatakuwa tayari kuona mali za umma zinaendelea kuharibika na kukwamisha nia njema ya serikali kwa wananchi wake na maendeleo ya nchi.Huku akiweka wazi kuwa watumishi wasio waadilifu na waaminifu wanaotumia fedha za wananchi na serikali kwa maslahi binafsi ni bora waachie ngazi wenyewe kabla ya kuwakuta mambo wasiyo tarajia.
