Saudi Arabia imekataa kupokea "vitisho vya kisiasa na kiuchumi" juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, idara ya habari ya Saudi Arabia imearifu.
Taifa hilo limeeleza kuwa linaweza kujibu shinikizo lolote kwa kuchukua hatua kubwa zaidi, mmoja wa maafisa wa juu ambaye jina lake alifahamiki alisema." Khashoggi, ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudi Arabia alitoweka Oktoba 2 katika mazingira ya kutatanisha baada ya kutembelea ubalozi wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki"
Rais wa Marekani Donald Trump alidai kuiadhibu Saudi Arabia kama itabainika kuwa nchi hiyo imehusika kumuua mwandishi huyo.
Aidha mamlaka ya Istanbul inaamini kwamba Khashoggi aliuawa alipokuwa anajadiliana na watu kutoka Saudi Arabia hivyo kukataa malalamiko hayo ni uongo.
