Nov 9, 2018

Ajibu ajipa kibarua kigumu Yanga


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu amesema kuwa bado hajaridhika na mafaniko ambayo ameyapata kwa kuwa ligi bado inaanza na inabidi afanye mambo makubwa kuliko hayo.

Ajibu ambaye kwa sasa anaongoza kwa kutoa pasi nyingi za mabao akiwa ametoa 9 na kufunga mabao 3 kati ya 17 ambayo wamefunga Yanga amesema kazi kwake ndo inaanza.

"Hakuna kikubwa kinachonifanya nifurahie kufanya hivyo kwa kuwa ni kazi yangu, bado ninajitahidi kuongeza juhudi ili kufanya makubwa zaidi ya hapa nilipofika kwa sasa, mashabiki waedelee kutupa sapoti," alisema.

Yanga wamecheza michezo 10 na kufanikiwa kuwa na pointi 26 sawa na wapinzani wao Simba wakizidiwa kwa mabao 6 na Simba ambao wapo nafasi ya pili wakiwa wamecheza michezo 11.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger