Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi jijini Mwanza, amewataka wananchi wa Kata ya Mbugani kutokuingilia kazi ya mahakama inayosubiriwa kutoa hukumu ya mgogoro wa muda mrefu wa Shule ya Msingi Mbugani kati ya wananchi wa Mbugani na BAKWATA.
Dk. Nyimbi amesema hayo katika Kikao cha Serikali amani dhidi ya mgogoro wa wananchi BAKWATA, amesema kuwa historia inaeleza mwaka 1967 Shule ya Msingi Mbugani, Bugando na St. Augustine zikichukuliwa na Serikali na baadaye Shule ya Msingi Mbugani ilirudishwa kwa BAKWATA na wanafunzi waliokuwa wanasoma katika shule hiyo hawakuandikisha wengine mpaka walipomaliza Darasa la Saba la Mwisho Mwaka 2016 na shule ikabaki wazi, ambapo wananchi walipeleka kesi mahakamani na kuwaomba wananchi na BAKWATA wawe na amani sheria itafuata mkondo wake mwenye haki atapata.
"Kwa kuwa historia inaeleza hivyo mimi sina mamlaka ya kuingilia kesi ambayo iko mahakamani na kilichobaki cha msingi ni kuwaomba kusubiri hukumu hiyo itakayotolewa na mahakama mnano, Februari 12, 2019 hapo ndio kila mmoja atakuwa huru kufanya chochote kilichobaki kwa sasa ni kuwa na amani na kushirikiana na katika shughuli za ujenzi wa Taifa, amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba amesema kuwa halmashauri ina jumla ya shule 80 za msingi ambapo Shule ya Msingi ya Mbugani haipo katika idadi hiyo, ambapo ametaka pande moja kati ya zote mbili kwenda mahakamani kuomba zuio la pande yoyote kutokujihisha na shughuli zozote katika shule na eneo hilo ili kupunguza mgogoro huo katika eneo la Mbugani mpaka pale suluhu pale itakapopatikana.
Naye Diwani wa Kata ya Mbugani jijini Mwanza, Mahmoud Gombe Gombe, amebainisha alipokea mkataba ulionesha kuwa Januari 1, 2017 shule hiyo ikabidhiwe BAKWATA lakini bado hawajakabidhiwa, kwani mkataba ulieleza mali zilizomo ni za halmashauri kwa hiyo majengo ndio wapewe BAKWATA, ambapo amesema kuwa kutokana na sintofahamu hiyo ndio chanzo cha mgogoro huo.
Hata hivyo Mjumbe wa Kamati ya Halmashauri Mkoa BAKWATA, Nurdin Mbaji amesema kuwa baada kupata maagizo toka ofisini kwake kuhusu kuhakiki mipaka ya eneo hilo alifika na Idara ya Mipango Miji kisha kumshirikisha Mwenyekiti wa Mtaa na ambaye alimkabidhi Mjumbe wawe nae katika kuhakiki mipaka hiyo, ndipo wananchi walileta vurugu na kuzuiliwa na kuendelea na zoezi hilo.
"Nilienda kutoa taarifa Ofisini kwangu na kunisihi nitulie mpaka ilipofikia jana wananchi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo walienda kufunga na makufuli ofisi zetu, na sisi tulipokuja katika ofisi yetu tulikuta kufuli na shughuli zetu zikasitishwa kwa muda kutokana na changamoto hiyo, iliyochukuwa muda mrefu hatimaye akaja kijana mmoja kutoka upande wao kuja kutufungulia, ameeleza Mbaji.
Aidha Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbugani Benard Wegoro, amesema kuwa BAKWATA walimpigia simu wakimuambia awaandikie barua kwa ajili ya kwenda kuhakiki mipaka ya eneo la shule hiyo, ambapo aliwakatalia na kuwaambia suala hilo lipo mahakamani na kuwataka wasubiri mahakama watakakapo toa suluhu, na kubainisha kuwa baadhi ya majengo ya shule hiyo yalijengwa na wananchi ambao wanasubiri hukumu ya shule hiyo.
