Peter na Paul Okoye waliokuwa Psquare wamjibu kaka yao

Leo Novemba 18, Peter na Paul Okoye waliokuwa wakijulikana kama  Psquare wanaadhimisha kuzaliwa kwao. Wawili hao wamezaliwa Novemba 18 mwaka 1979 ambapo leo wanasherekea miaka 39 ya uhai wao.

Kaka yao mkubwa Jude Okoye  ambaye ni Mtendaji maarufu wa muziki alituma picha ikiwaoneesha enzi za utoto wa Peter na Paul kwenye mtandao wa Instagram ikiashiria kwamba ameweka kando tofauti alizokuwa nazo hapo awali  kwa Peter. Katika picha hiyo, Jude aliandika  ‘Happy birthday to @rudeboypsquare @peterpsquare ???More life ??.’