Na. Thabit Madai,zanzibar.
WANAHARAKATI wa kutetea haki za Wanawake nchini wametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria ili kukamilisha kesi za mauwaji ya wanawake na watoto kwa wakati muafaka.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) upande wa zanzibar, Dk Mzuri Issa Ali katika taarifa yake kwa vyombo vya habari wakati dunia vya ukatili wa kijinsia ambapo inaadhimisha siku 16 za kupinga vitendo,
Dkt, Mzuri Alieleza kuwa kama kesi hizo zikishughulikiwa kwa haraka na taarifa zake kusambazwa nchini kote itapunguza tabia ya baadhi ya watu ya kuendelea na tabia hiyo kumaliza maisha ya wanawake na watoto nchi.
Alisema kwa mwaka huu pekee, tayari wanawake watano na watoto wawili wameripotiwa kuuawa katika mkoa wa Kusini Unguja lakini bado kesi hizo hazijapatiwa wowote hadi leo.
Alieleza kwamba Mei 14, 2018 mtoto Elizabeth Ndaula mwenye umri wa miaka 8 alikutwa amefariki katika kichaka huko Bambi wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja pia Mei 22, 2018 Patima Abdallah Makame (27) na mtoto wake wa miezi mitano Haji Ismail walikutwa wameuawa nyumbani kwao Guruweni Jendele wilaya ya Kati.
Julai 18 na 31, 2018 msichana Wasila Mussa (21) wahuko Tunguu Kichangani Wilaya ya Kati pia mwizi huo huo na Agatha Francis Pius mkaazi wa Kiboje Ndagaa wilayani humo aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye makali shingoni kwake wakati akienda shamba saa nne asubuhi.
Novemba 2. 2018 majira ya saa 7:00 usiku Issa Masuli Juma (40) na mkewe Asha Khamis (20) wote wakaazi wa Kibele wilaya ya kati waliuliwa na watu wasiojulikana kwa kupigwa na kitu kigumu sehemu ya kichwani nyumbani kwao.
Dk. Mzuri alieleza kuwa kila wakiwasiliana na jeshi la Polisi wanajibiwa kuwa uchunguzi uendelea na bado haujakamilika na ukikamilika watafikishwa mahakamani, Maadhimisho hayo huadhimishwa kila mwaka kuazia Novemba 25 hadi Desemba 10.

