Golikipa wa Yanga alazwa Hospital

Kabwili akiwa amelazwa

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Samwel Lookmay, amesema Golikipa ya wa Yanga Ramadhani Kabwili,  bado yupo hospitali madaktari wakiendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini ukubwa wa tatizo lake.

"Kabwili alipata matatizo kwenye nyonga na sasa hivi bado yupo chumba cha CT Scan akifanyiwa uchunguzi ili kugundua tatizo ni nini , lakini misuli ilibana na kupelekea kushindwa kabisa kuendelea na mchezo", amesema Samwel Lookmay,

Aisha kaimu Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa kinachosubiriwa kwasasa ni taarifa kutoka kwa daktari ili kujua ni nini kitaendelea ama kama ataruhusiwa kutoka.
Mpya zaidi Nzee zaidi