Kesi ya Zitto kuhusu Spika na CAG yapigwa kalenda


Kesi iliyofunguliwa na Bunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe Mahakama Kuu dhidi ya Spika wa Bunge Job Ndugaiimeahirishwa hadi Februari 15 mwaka huu itakapo sikilizwa tena.

Kesi hiyo ya Kikatiba namba 01/2019 imefunguliwa na Zittokuomba tafsiri ya Mahakama kuhusu madaraka ya Bunge kumuita na kumuhoji CAG.

Utakumbuka kesi hiyo ni baada ya Spika Ndugai kumtaka CAG, Prof. Assad kufika mbele ya kamati hiyo Januari 21, mwaka huu, kujieleza kuhusu kauli yake aliyoitoa akiwa nchini Marekani kuwa ‘Bunge ni dhaifu’, wito ambao CAG, Prof. Assad aliuitikia.
Mpya zaidi Nzee zaidi