Mr. Blue amalizana na Diamond


Msanii wa Bongo Fleva, Mr. Blue amesema  ameachana na kutumia jina la Simba ambalo kwa sasa limeonekana likitumika zaidi na Diamond na Platnumz.

Muimbaji huyo kwenye Mahojiano na Wasafi TV amesema kwa wakati huo anatumia jina la Nyani
Mzee badala ya lile la Simba.

"Sisi wote binadamu tunapenda tunaishi, ndugu yangu msanii (Diamond), Afande Sele msanii fresh. Na sasa nina a.k.a yangu mpya Nyani Zee, kwa sababu nyani hadi azeeke kakwepa mishale mingi," amesema Mr. Blue.

Kwa sasa Mr. Blue anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina Blue ambao amemshirikisha muimbaji Nandy.

Mpya zaidi Nzee zaidi