Mshambuliaji wa Simba SC, John Bocco sasa amerejea rasmi na atacheza mechi dhidi ya Al Ahly.
Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems amesema hali ya mchezaji huyo inaendelea vema kwa sasa na kuna uwezekano akawa sehemu ya kikosi dhidi ya Al Ahly itakayopigwa Februari 2, mwaka huu nchini Misri.
Bocco aliumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ambapo walishinda goli 3-0.
