Loading...

2/12/2019

Lady Jaydee ajitolea kuwasaidia wanafunzi


Msanii wa Bongo Fleva, Lady Jaydee amejitolea kuchagia ujuenzi wa mabweni katika shule ya sekondari ya Lamadi.

Muimbaji huyo huyo nguli ameeleza kuwa shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi kama ukosefu wa vyoo vya kutosha, pedi za kujikimu wakati wa hedhi kwa watoto wa kike na mabweni.

"Mimi binafsi nimeguswa na kuahidi kushughulikia swala la mabweni, ili kuwaepusha na vishawishi vya bodaboda na Chips huko barabarani," ameeleza Lady Jaydee.

Lady Jaydee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo, Too Late ametoa wito kwa wadau wote watakaoguswa washirikiane kufanikisha kutatua changamoto hizo ili wanafunzi hao waweze kusoma vizuri na katika mazingira mazuri.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger