Mahakama zinazotembea kuzinduliwa leo, Rais Magufuli atajwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo anatarajia kuzindua Mahakama zinazotembea (Mobile Court) Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania, Eva Nkya uzinduzi huo utafanyika katika sherehe za siku ya Sheria kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC).
Mpango huo umekuja kufuatia maombi ya Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma kwa Rais Ikulu January 29 mwaka huu wakati akiwaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ombi lililohusu kuimarisha miundombinu ya Mahakama.