Rais wa TLS, Fatma Karume kutohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria


Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume hatohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria February 6 mwaka huu baada mahakama kumwambia kuwa hatoweza kuhutubia kutokana na ufinyu wa muda, awali alipewa mwaliko, na kutakiwa kuandaa hotuba yake kwa ajili ya maadhimisho hayo.

Amesema kuwa aliandaa hotuba inayoendana dhana ya sherehe za mwaka huu na aliiwasilisha kwa sekretarieti ili aweze kupata maoni kutoka TLS, mnamo February Mosi mwaka huu mahakama iliomba kupitia hutuba hiyo na aliituma kwa njia ya baruaa pepe kwa kutimiza wajibu wake.

"Leo nimepokea barua inayosema mimi, TLS na Mwanasheria mkuu wa Serikali hatutoweza kuhutubia UMMA kutokana na ufinyu wa muda," amesema Fatma.

Utakumbuka mwaka jana aliyekuwa Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu alishindwa kuhudhuria kutokana na hali ya ugonjwa na alikuwa anaendelea na matibabu nje ya nchi.