Matunzo ya watoto yatajwa kuwa ni janga


Na Ahmad Mmow Ruangwa.

Huduma na matunzo kwa watoto katika mkoa wa Lindi vimetajwa kuwa ni tatizo kubwa linaloelekea kuwa janga kutokana na kushindwa kumalizika.

Hayo yameelezwa leo na mratibu wa mradi wa kuboresha huduma za msaada wa kisheria wa shirika la msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto wa  Lindi(LIWOPAC),Fatuma Nyama  wakati wa mkutano wa wadau wa huduma za msaada wa kisheria,uliofanyika mjini Ruangwa.

Nyama alisema tatizo la matunzo kwa watoto nikubwa mkoani humu kiasi cha kueguka kuwa janga kutokana na kutomalizika,japokuwa kumekuwa na juhudi kubwa ya kutoa elimu kwa jamii.

Mratibu huyo wa mradi alisema kupitia vituo vya msaada wa kisheria,kesi mbalimbali zimeripotiwa kwa wasaidizi wa kisheria.Ambapo mwaka jana jumla ya kesi 622 ziliripotiwa.Huku kesi za matunzo kwa watoto  zikiongoza kuripotiwa kwenye vituo hivyo vilivyo chini ya LIWOPAC.

"Hili limekuwa janga kubwa katika mkoa wetu.Hivyo kama shirika tumechukua hatua za makusudi kuelezea ukubwa wa tatizo hili," alisema Nyama.

Alisema akina mama wengi wanakwenda kulalamika kuhusu matunzo ya watoto kutoka kwa mababa wa watoto hao.Hali iliyosababisha katika kesi hizo zilizoripotiwa,489 zimeripotiwa na wanawake.

Alitoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu utoaji elimu ili kukomesha tatizo hilo.Akiweka wazi kwamba madhara ya tatizo hilo nimakubwa.Ikiwamo kuporomoka kwa viwango vya ufaulu  kutokana na utoro unaosababishwa na kukosa huduma muhimu.

Aidha Ofisa huyo wa LIWOPAC alisema kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka Jana,watu 93,858 LIWOPAC limeweza kuwafikishia elimu ya kisheria.Ambapo kati watu hao,45,630 ni wanawake.Wakati 48,228 ni Wanaume.

Mpya zaidi Nzee zaidi