Loading...

2/12/2019

Watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto Njombe wapandishwa kizimbani (+Picha)


Watuhumiwa watatu wa utekaji na mauaji ya watoto wilayani Njombe wamefikishwa katika Mahakama ya Hakim Hakimu mkazi Njombe leo.

Hatua hiyo imekuja siku moja mara baada ya Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na
Usalama, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania CDF, Jenerali Venance Mabeyo kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kuona mwenendo wa matukio ya utekaji na mauaji ya watoto.
utakumbuka kuwa mwishoni mwa January mwaka huu  Watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 walipatikana wakiwa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani humo.

Hata hivyo hivi karibuni serikali kupitia  Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ilisema kuwa tayari watu 29 wanashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia mauaji hayo.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger