Inaripotiwa kuwa kikosi cha Yanga SC tayari kipo kambini mjini Morogoro kwa ajili ya kujiaandaa
na mchezo wao dhidi ya Simba SC.
Yanga SC na Simba SC wakutana kwenye dimba la uwanja wa Taifa February 16 mwaka huu katika
mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ((TPL).
Wakati Simba wanashuka dimbani leo kuwavaa Al Ahly kutoka kutoka nchini Misri kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga tayari wameanza kupashwa misuli moto kwa ajili ya mchezo wao huo utakaochezwa Jumamosi hii.
Hadi sasa Yanga SC inaongoza Ligi ikiwa imejikusanyia pointi 58 katika michezo 23 waliyocheza, wakati wapinzani wao, Simba SC wakiwa na pointi 36 pekee kibindoni walizokusanya katika michezo 15 waliyocheza.
