![]() |
| Katikati Waziri Kairuki |
Amesema hayo mara baada ya kupokea ujumbe wa raia saba wa Hongkong China waliowasili Nchini wakiwawakilisha wafanyabiashara wa nchi hiyo waliokuja kufanya utafiti wa maeneo ya kuwekeza.
“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaimarisha uwekezaji, mpango huo ambao ulifanyika Mei mwaka jana unalenga kuondokana na vikwazo vya kibiashara na kuharakisha vibali na kutoa ardhi kwa ajili ya uwekezaji, tunayafanya haya ili kuongeza ufanisi katika sekta ya uwekezaji, tunataka Watanzania wanufaike,” amesema Waziri Kairuki.
Ujio wa Wajumbe saba kutoka Hongkong Nchini China ni sehemu ya wafanyabiashara wengi kutoka Jijini humo wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania hatua ambayo imekuja kufuatia kuwepo kwa hamasa ya uwekezaji na kuimarishwa kwa mazingira hayo nchini.
