Waziri Lugola kufanya ziara ya siku 10 Arusha


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili jijini Arusha leo, kwa ajili ya kuanza
ziara yake ya kikazi ya siku kumi kwa kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo ili kusikiliza kero za
wananchi.

Mara baada ya kuwasili amesema baada ya kuzungumza na Askari na Watumishi wa Wizara yake
pamoja na kupokea changamoto zao, atafanya mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi
utakaofanyika katikati ya Jiji hilo ili wananchi wengi waweze kufika na kueleza kero.

“Wananchi wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kusikiliza matatizo yao yanayowakabili, ndio
maana nimepanga kufanya ziara kama hizi nchi nzima, hii inasaidia sana kujua matatizo
mbalimbali ya wananchi pamoja na kuangalia utendaji kazi wa Taasisi zangu zilizopo ndani ya
Wizara hii," amesema Waziri Lugola.

Waziri Lugola anatarajia kuanza ziara hiyo rasmi kesho jijini humo kwa kukutana
na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kupokea taarifa ya Kamati
hiyo, kabla ya kuanza kuzungumza na Wakuu wa vyombo vyake na baadaye atakutana na Kamati ya
Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa, na kumaliza kwa kuzungumza na Baraza la Askari na
Watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo jijini humo.
Mpya zaidi Nzee zaidi