Maafisa wasiopungua 26 wa kikosi cha zimamoto wamefariki baada ya kutumwa kuzimwa moto wa msituni katika eneo la mbali kusini-magharibi mwa mkowa wa Sichuan nchini China mwishoni mwa wiki.
Maafisa wamesema mamia ya askari wa zimamoto walipelekwa kupambana na moto uliozuka Jumamosi jioni katika kaunti ya Muli, kulingana na wizara inayoshughulikia matukio ya dharura.
Maafisa walipoteza mawasiliano na askari 30 wa zimamoto jana Jumapili, baada ya mabadiliko ya ghafla ya mwelekeo wa upepo kusasabisha mripuko mkubwa wa moto.
Rais Xi Jinping na waziri mkuu Li Keqiang wametoa maagizo kushughulikia dharura hiyo.
