Maalim Seif ajibu kuhusu kugombea Urais


Makamu wa kwanza wa Rais (Mstaafu) wa Zanzibar, Maalim Seif ambaye hivi karibuni ameamia Chama cha ACT Wazalendo amejibu iwapo yupo tayari kugombea urais.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV amesema bado wakati wa kuweka bayana hilo haujafika.

"Kwenye siasa siku Moja ni kubwa sana suala hilo muda wake haujafika, nitawaambia," amesema Maalim Seif. 

Katika hatua nyingine, Maalim aliongeza kuwa, 'Tuliwaambia wale wanaotaka kujiunga na ACT waje wajiunge na wengi walinifuata, mpaka sasa sijarudisha kadi ya CUF, tulishakubaliana kuwa kadi, nguo na kila kitu cha CUF tutampelekea msajili'.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items