Waongoza watalii Mlima K'njaro kuokolewa bure kwa Helkopta


Shirika la Kilimanjaro SAR linayojishughulisha na utoaji wa huduma ya utafutaji na uokoaji wa watalii wanaopata matatizo ya kiafya katika maeneo yenye muinuko ikiwemo Mlima Kilimanjaro limetangaza kutoa bure huduma zake waongoza watalii pamoja na wapagazi.

Huenda taarifa hizi zikawa faraja kwa kundi hili la Waongoza Watalii pamoja na wapagazi maarufu kama Wagumu ambao wanatajwa kama wadau muhimu zaidi katika utalii wa kupanda Mlima kwa kuhakikisha safari ya watalii ya kupanda mlima inamalizika salama.

Licha ya malalamiko yao ya muda mrefu juu ya ujira mdogo wa kiasi cha sh 5000 hadi 8000 wanazolipwa na kampuni wanazo fanya nazo kazi, bado kundi hili limekuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za Afya hali inayochangiwa na kipato kidogo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items