Uchaguzi wa Yanga SC unatarajiwa kufanyika Mei 5 mwaka huu na Fomu zitaanza kutolewa Kesho Makao Makuu ya Klabu hiyo. Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Malangwe Ally Mchungahela ndiye ametangaza tarehe hiyo.
Awali uchaguzi huo ulitangazwa kufanyika Aprili 28 lakini kutokana na siku hiyo itakuwa fainali ya michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.
Ratiba kamili ya uchaguzi wa Yanga.
Aprili 2-7 kuchukua fomu
Aprili 9 Kikao cha mchujo kwa wagombea
Aprili 10 kubandikwa kwa majina yaliyopitishwa
Aprili 11-14 Pingamizi kwa wagombea
Aprili 16-18 Kupitia pingamizi na usaili
Aprili 18-23 Sekretariati kusikiliza maamuzi ya kamati ya maadili
Aprili 24-26 Kukata rufaa
Aprili 27-29 kusikiliza rufaa
Aprili 30- Mei 4 Kampeni
Mei 5 uchaguzi mkuu
