Katibu Mkuu Wizara ya Habari Bibi.Susan Mlawi na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii wakutana kuzungumza namna ya kutumia fursa mashindano ya AFCON U- 17 yanayotarajia kuanza mapema mwezi Aprili kutangaza fursa za Utalii.
Katika Mkutano huo Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw.Wilfred Kidao alisema kuwa katika ufunguzi wa mashindano hayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Bw.Gianni Infantino anatarajia kuwepo.


