Lady Jaydee afunguka kuhusu Clouds Media, Ruge Mutahaba


Msanii wa muziki Bongo, Lady Jaydee amefunguka na kueleza kuwa hajawahi kufuatilia iwapo Clouds Media wameanza kucheza nyimbo zake.

Muimbaji huyo anayetamba na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la I Don't Care, amefunguka hayo kwenye kipindi cha Block89, Wasafi FM.

"Sijawahi kusikia au kuambiwa kama Clouds Media wameanza kupiga ngoma zangu," amesema Lady Jaydee.

"Nilibadilisha jina la Profile na kuandika 'I dont care' kabla hata matatizo hayajatokea, ila matatizo yalivyotokea ndio kila mtu akaanza kuiona hiyo "I don't care"

Ameendelea kwa kusema, "Nilianza promotion kabla ya msiba wa Ruge Mutahaba, lakini ulivyotokea ikabidi nitulie, watu ukifanya kitu wanatukana usipofanya wanatukana vilevile"