Miongozo ya matumizi sahihi ya TEHAMA Serikalini yapitiwa


Mkutano wa siku mbili wa Maofisa TEHAMA (ICT) kutoka wa Wizara ya Afya, Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma umefunguliwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Edward Mbanga Jijini Dodoma.

Lengo la Mkutano huo ni kupitia miongozo ya matumizi sahihi ya TEHAMA Serikalini ili kuongeza ufanisi wenye tija katika matumizi ya TEHAMA utaosaidia kuboresha utoaji huduma katika Sekta ya Afya nchini.

Mbali na hayo kikao hicho kimelenga kupitia changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo Wataalamu hao katika utoaji huduma na kutoa mapendekezo ya kutatua changamoto hizo ili kuboresha utendaji wao katika Sekta ya Afya.

Hata hivyo kikao hicho kilichowakutanisha Wataalamu wa masuala ya TEHAMA kimekusudia kujenga uelewa wa pamoja baina ya Wataalamu hao hususan katika masuala ya Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na matumizi sahihi ya TEHAMA Serikalini.

Kwa upande mwingine Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ambae pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Edward Mbanga amepongeza uwepo wa mkutano huo jambo litalosaidia kuiboresha zaidi taaluma hiyo, hovyo kuahidi kumwalika Afisa Mwandamizi wa Idara ya Utawala ataesikiliza na kutatua changamoto zinazowakumba.