Shirika la ndege la Kenya latangaza hasara


Shirika la taifa la safari za ndege nchini Kenya, Kenya Airways(KQ) limetangaza kupata hasara ya kifedha mwaka uliopita kwa takribani dola za kimarekani milioni 75 ambayo ni sawa na Bilioni 7.55 ya Kenya.

KQ inasema kuwa hasara imetokana na ongezeko kubwa bei ya mafuta, mishahara ya juu, migomo na viwango vya juu vya gharama za usafiri wa ndege.