Mambo yatakayokushangaza kuhusu mwili wako



Inawezekana unatazama mwili wako kwa juu juu pekee bila kufahamu mambo mengi yaliyojificha kwenye mwili wako. Ni hakika kuwa mwili umeumbwa kwa namna ya pekee sana inayouwezesha kufanya kazi pamoja na kuonekana jinsi ulivyo.

Naamini unapenda kupata maarifa kwa kuufahamu mwili wako vyema. Karibu ufuatilie makala hii ili nikujuze mambo  yakukushangaza kuhusu mwili wa binadamu.

1. Ubongo unatumia asilimia 20 ya oksijeni pamoja na kalori
Ni wazi kuwa utendaji kazi wa ubongo unahitaji oksijeni asilimia 20 pamoja na kalori kutoka kwenye mwili ili kufanya kazi jinsi ipasavyo.Ubongo

2. Kila mtu ana harufu yake
Mbali na mapacha wa kufanana, kila mtu ana harufu yake ya pekee inayomtofautisha kati yake na mtu mwingine.

3. Uwezo mkubwa wa kufikiri unahusiana na kiasi cha ndoto mtu anazoota.
Inaaminika kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri (Intelligent Quotient – IQ) huota ndoto nyingi zaidi kuliko watu wenye IQ ndogo. Hili kwako likoje? Naamini utatupa maoni yako hapo chini.

4. Wanawake hupepesa macho zaidi kuliko wanaume.
Inaaminika kuwa wanawake hupepesa macho (blink) mara mbili zaidi kuliko wanaume.

5. Wanaume hupata kwikwi kuliko wanawake.
Kwikwi ni mkazo wa ghafla na usio wa hiari wa misuli ya kiwambo unaosababisha pumzi kutokea kinywani na sauti ya kugugumia kutokana na hewa kuingia kwenye umio. Hivyo tafiti zimebaini kuwa wanaume hupata kwikwi mara mbili zaidi ya wanawake.

6. Unaweza kujaza bwawa la kuogelea kwa mate yako.
Bwawa la kuogelea? Ndiyo, kwa kipindi cha maisha yako yote unazalisha kiasi cha mate kinachoweza kujaza bwawa la kuogelea kama kingekuwa kinakusanywa.Mtoto

7. Ukishiba sana hausikii vizuri
Utafiti umebainisha kuwa uwezo wa kusikia hupungua pale mtu anapokuwa ameshiba sana. Labda hii ndiyo sababu watu wengi hawawi wasikivu baada ya kula sana; hasa wanafunzi shuleni.

8. Mtoto mchanga hutambua rangi nyeusi na nyeupe pekee
Inaelezwa kuwa mtoto mchanga hatambui rangi nyingine zaidi ya nyeusi na nyeupe pekee. Hii ni kusema kuwa ulimwengu wote kwa mtoto ni mweusi na mweupe pekee.

9. Konea ni sehemu ya jicho isiyopelekewa damu
Konea (cornea) sehemu angavu ya mbele kwenye jicho. Hii ni sehemu pekee kwenye mwili isiyokuwa na damu; sehemu hii hupata oksijeni moja kwa moja kutoka kwenye hewa.Konea

10. Asilimia 75 ya ubongo ni maji
Naamini unafahamu kuwa asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji. Lakini je wajua kuwa asilimia zaidi ya 75 za ubongo wa binadamu ni maji? Fahamu hili sasa.


11. Nywele zinaweza kuishi kwa miaka 3 hadi 7
Je wajua kuwa nywele za binadamu ni sehemu hai ya mwili? Nywele za binadamu zinaweza kuishi kwa miaka 3 hadi 7.

12. Meno huanza hukua miezi 6 kabla ya kuzaliwa
Ingawa mtoto mchanga napozaliwa meno yake yanakuwa bado hayajachomoza kwa nje, lakini yanakuwa tayari yameshaanza kuota kwa ndani miezi sita kabla ya kuzaliwa.

13. Figo yako ina vichujio milioni moja
Kila figo yako moja ina vichujio takriban milioni moja vinavyochuja lita 1.3 za damu kila dakika na kupelekea kuzalisha lita 1.5 za mkojo kwa siku.Figo

14. Binadamu wengi hawawezi kuchezesha masikio yao
Inasemekana ni watu wachache pekee ndiyo wanaoweza kuchezesha masikio yao duniani. Je wewe unaweza? Ikiwa unaweza basi uko kati ya hao wachache.

15. Pua ya binadamu inaweza kubaini harufu trilioni moja
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Leslie Vosshall kwenye chuo cha Rockefeller, ulibaini kuwa pua ya binadamu inaweza kubaini harufu tofauti takriban trilioni moja. Kiwango hiki ni tofauti na kilichokuwa kinafahamika mwanzo cha harufu 10,000. Je wewe unajua ulishanusa harufu ngapi? Kama unajua basi tuandikie hapo chini.

16. Ndevu za mwanaume zinaweza kufikia mita tisa
Inaelezwa kuwa ikiwa mwanaume hatonyoa ndevu katika maisha yake yote; ndevu zake zinaweza kukua na kufikia urefu wa mita tisa.

17. Binadamu ana misuli zaidi ya 600
Mwili wa binadamu una misuli kati ya 600 hadi 800. Pia inahitajika misuli 200 ili kuweza kupiga hatua moja.Misuli

18. Unaweza kuishi siku 30 bila chakula
Inaelezwa kuwa binadamu anaweza kuishi siku 30 bila chakula; siku 3 bila maji; dakika tatu bila oksijeni. Je ulilifahamu hili kuwa unaweza kunywa maji tu bila kula na ukaishi siku thelathini?

19. Unaweza kukaa bila kulala kwa siku 11
Rekodi ya dunia ya mtu aliayeweza kukaa muda mrefu zaidi bila kulala iliwekwa na Randy Gardner ambaye alikaa siku 11 pekee. Inaelezwa kuwa ukikaa zaidi ya hapa utaanza kupata matatizo ya kiakili na kisaikolojia.

20. Mawimbi kwenye mfumo wa fahamu husafiri kwa kasi ya mita 120  kwa saa (kilometa 200 kwa saa)
Inaelezwa kuwa unapomgusa mtu au kitu kinapomgusa mtu, tarifa za tendo hilo husafiri kwa kasi kubwa ya mita 120 kwa saa (kilometa 200 kwa saa) kuelekea kwenye ubongo.

21. Binadamu huvuta hewa mara 23,000 kwa siku
Waatalamu wa afya wanaeleza kuwa binadamu huvuta hewa takriban mara 23,000 kwa siku moja.Kupumua

22. Mwili wako una kaboni nyingi sana
Inaelezwa kuwa mwili wako una kaboni nyingi kiasi cha kutosha kuzalisha penseli 900 ikiwa kaboni hiyo itakusanywa.

23. Ubongo unaweza kutunza kiasi kikubwa cha kumbukumbu.
Kwa kipindi cha maisha ya binadamu yote, ubongo wake unaweza kutunza biti za data zipatazo milioni bilioni moja. Milioni bilioni moja? Ndiyo, milioni bilioni moja na zaidi.

24. Moyo unaweza kuendelea kudunda hata ukiwa nje ya mwili
Nini? Ndiyo, moyo unaweza kuendelea kudunda hata ukiwa nje ya mwili ikiwa tu utapata oksijeni. Moyo umeumbwa kwa namna ambayo unazalisha mawimbi yake ya umeme wenyewe yanayowezesha misuli yake kusukuma damu. Hii ndiyo sababu wataalamu wa tiba wanaweza kuutoa moyo na kuurudisha tena bila shida.Moyo

25. Kidole cha mwisho ni muhimu sana
Ikiwa mtu atakikosa kidole cha mwisho au kidogo cha mkono wake, basi nguvu za mkono wake zitapungua kwa asilimia 50.

Naamini umejifunza mengi na kufurahia makala hii. Ni wazi kuwa kuna mambo mengi yakushangaza kuhusu miili yetu ambayo nisingeweza kuyaeleza yote hapa. Lakini naamini kwa mwanzo huu utapata hamasa ya kufanya utafiti zaidi juu ya mengine mengi.