Picha: Serikali yatoa Motisha kwa wanafunzi bora, Shule zilizofanya vizuri 2018

Miongoni mwa wanafunzi bora wa Kidato cha Sita mwaka 2018 tokea Shule ya Sekondari Mvumi, Erick Maximilian akipokea cheti na zawadi pesa taslimu shilingi milioni 1.5 toka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 jijini Dodoma. Pamoja na kuwa mwanafunzi huyo kuwa ni mwenye mahitaji maalum

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Avemaria Semakafu akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018  jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato ya jijini Dodoma wakifuatilia hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu

Meneja wa Shule ya Kaizirege and Kemebos toka Bukoba,Eulogius William akipokea cheti na tuzo toka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako kutambua mchango wa Shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mwaka 2018 wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 jijini Dodoma

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya hafla ya Siku ya Elimu ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 mara baada ya kumaliza hafla hiyo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu