Serikali kumlipa fidia mwanamke aliyemeza ARV kwa miaka 5 kwa kupewa majibu ya uongo kuwa ana UKIMWI


Mwanamke mmoja nchini Malawi ambaye alimeza dawa za kutibu makali ya ugonjwa wa UKIMWI kwa muda wa miaka mitatu baada ya kupewa matokeo yasiyokuwa sahihi ya ugonjwa huo, sasa anatarajia kulipwa fidia na serikali.

Bi. Agnes Jumbe alipewa matokeo ya kupotosha na kuwekwa kwenye mpango wa kumeza dawa za ARV baada ya kupimwa katika hospitali ya serikali mwaka wa 2014.

Mawakili wake waliambia mahakama ya Lilongwe kwamba mwanamke huyo alipitia wakati mgumu mno katika kipindi hicho ikiwemo kutalakiwa na mume wake. Jaji Ivy Kamanga ambaye alikuwa akiwakilisha serikali alikubali kuwa serikali italipa mwanamke huyo fidia.