Wanawake wagoma wakitaka usawa mishahara


Wanawake nchini hapa wamefanya mgomo kazini kupinga kile wanachodai ni kutokuwapo usawa wa kijinsia hususani katika mishahara. Hawakwenda kazini badala yake waliandamana mtaani pamoja na kwenda mbele ya jengo la serikali mjini Bern kushinikiza mabadiliko.

Mgomo huo wa jana umekuja miaka 28 baada ya kufanyika mwingine wa namna hiyo mwaka 1991 uliohusisha wanawake wapatao 500,000 . Wanawake nchini wamekuwa katika kampeni ya muda mrefu kuharakisha usawa wa kijinsia. Waliungana na mamilioni ya wanawake wa Ulaya baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia iliyomalizika mwaka 1918 wakitaka haki ya kupiga kura ambayo hawakuipata hadi 1971.

Wakati wa mgomo mwaka 1991, hapa kuwa na mwanamke yeyote aliyekuwa katika serikali ya Uswisi kuwa na sheria yoyote ya kuruhusu wanawake kwenda likizo ya uzazi. Mpaka sasa, wanawake nchini Uswisi hupata asilimia 20 pungufu ya kipato cha wanaume. Pia wana uwakilishi mdogo nafasi za juu uongozi. Mwezi uliopita, utafiti wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) uliiweka Uswisi nafasi ya chini ya orodha ya nchi zinazolipa kiwango kidogo kati ya wanawake na wanaume majukumu ya juu.

"Nafikiri baada ya hapa, hakuna kitu kitakachoshindikana,"alisema mwandishi wa habari, Beatrice Born ambaye mwaka 1991 alipokwenda kujifungua, aliporudi kazini hakutakiwa kuendelea na kazi yake. Mmoja wa waratibu wa mgomo wa mwaka 1991, Paola Ferro, alisema anashiriki mgomo huu mpya na sababu za kufanya hivyo ni haki ya kijinsia kama ilivyokuwa miaka 28 iliyopita.


Mpya zaidi Nzee zaidi