Wizara ya afya kujifunza kutoka Kijiji hiki kutokomeza vifo vya mama na mtoto


Na Amiri kilagalila

Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee,na Watoto, Dkt. Zainab Chaula amewasili katika Kijiji cha Uturo kilichopo katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kujifunza jinsi ambavyo Kijiji hicho kimeweza kuzuia vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua kwani zaidi ya miaka 20 hakuna kifo kilichotokea katika kijiji hicho.

Aidha inasemekana kuwa Juhudi hizo zimetokana na aliekuwa Mganga mfawidhi zahanati ya Uturo kuanzia mwaka 1993 mpaka 2017,  Bw. Wilson Chotamganga ambaye baada ya kufika kijijini hapo alikuta vifo vingi vilivyotokana na uzazi kwa wakina mama na watoto waliozaliwa ,na watoto hao wachanga walikuwa wakizikwa na wakina mama kwa siri pembeni ya nyumba zao .

Hata hivyo, imeelezwa kuwa baada ya Mganga huyo kugundua matatizo hayo ndipo alipoamua kuwatafuta wahudumu wa afya ngazi ya Jamii ambao ni wakinamama maarufu kama Makomandoo ambao hutoa huduma za afya ya uzazi katika jamii toka mama anapogundulika na ujauzito hufatiliwa na kushauriwa kwenye kituo cha afya mpaka atakapojifungua.

Dkt. Chaula amesema baada ya kutoka kijijini hapo Wizara yake itaandaa mkakati wa kutoa elimu hiyo kwa kuisambaza Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items