Taasisi za fedha zatakiwa kuwekeza kwa wakulima


Na Timothy Itembe, Mara

Taasisi za Fedha zimekumbushwa kuwekeza nguvu nyingi kwa wakopaji wa fedha za kilimo kwaajili ya kuwainua wakulima na kuongeza ajira pamoja na kupunguza umasikini kwa jamii.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na na moja wa wafanyabiashara mjini Tarime mkoani Mara Modekai Moseti kwa niaba ya wenzake  kwenye kongamano la Jumuiko la wafanyabiashara kutoka  Tarime,Sirari, Nyamongo na Rorya lililoandaliwa na Benki ya NMB kwaajili  ya kuwapa elimu ya kujenga niadhamu ya fedha kwenye biashara.

 Moseti alisema kuwa Taasisi nyingi za kifedha hapa nchini zinawekeza mara nyingi kiwangop chaq fedha nyingi kwa wafanyabiashara badala ya kuwekeza kwa wakulima ambao ndio wengi ili kuinua kiwango cha uzalishaji mazao.

“Baba wa Taifa mwali Julius Nyerere enzi ya uhai wake aliwahi kusema kuwa   kilimo ni uti wa mgongo kwa Taifa letu kwa hali hiyo taasisi za fedha zinatakiwa kuwekeza fedha nyingi katika kilimo ili kuinua wakulima katika uzalishaji mazoa kwa lengo la kutoa ajira pamoja na kuondoa umasikini kwa jamii,”alisema Moseti.

Meneja mwandamizi kitengo cha biashara Benki ya NMB Tanzania,Toyi Ruvumbagu alisema kuwa Katika kuhakikisha Benki ya NMB inaunga mkono serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli wafanyabiashara na wakulima wetu wanaelimishwa juu ya maswala ya kukopa na ulipaji kodi.

Kodi katika nchi zote Duniani zinategemea kodi na kodi ni misngi wa maendeleo ya Taifa  nimatumaini yetu kuwa mafunzo haya yatakuwa chahu kwa wafanyabiashara na mtakuwa walimu wazuri kwa wa kutoa elimu hii mlioipata ya  mafunzo mbalimbali ya kibiashara ikiwemo utunzaji fedha,utafutaji masoko ulipaji wa kodi. kwa wale ambao hawakuhudhuria.

Kwa upande wake Meneja Meneja NMB Banki Tawi la Tarime,Gadiel Sawe alisema kuwa Benki yake imefanya jumuiko la kibiashara kwa wafanyabiashara wa kati na wadogo lengo likiwa ni kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya Tano kuhakikisha wafanyabiashara wanapata faida na kulipa kodi ya serikali kwa mjibu wa sheria.

Sawe aliongeza kusema kuwa jumuiko  hilo ni kwaajili ya kuongea na wafanyabiashara na kutoa mrejesho wa Benki ya NMB juu ya kuwahudumia watu na wateja wake katika kuhakikisha kuwa huduma zetu zinaboreshwa
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items