Jamii yatakiwa kuchangamkia fursa ya kusajili laini kwa njia ya vidole


Na Timothy Itembe, Mara

Jamii imetakiwa kuchangamkia frusa zinazotolewa na serikali ikiwemo kusajili laini za simu kwa njia ya vidole kwa usalama zaidi wa watumiaji wa mitandao ya simu.

Hayo yalibainishwa jana na Afisa Tarafa ya Inchage, Jonadhani Machango wakati wa uzinduzi wa mnara mpya wa 4G tekenolojia ya mawasiliano ya simu za mkononi Togo Tarime mjini.

Machango alisema kuwa serikali imetoa frusa kwaajili ya watumiaji wa laini za mitandao ya simu za mkononi kusajili laini zao kwa watumiaji kwaajili ya usalama wao.

 Naye Meneja wa Togo kanda ya Ziwa, Daniel Mainoya alisema kuwa lengo la mnara huo ni kuwafikishia wananchi wa mikoani maendeleo ya kijamii kwa kasi zaidi kupitia TEHAMA ikiwemo tekenolojia ya mawasiliaono ya simu za mkononi.

“Mnara tunaouzindua hapa leo una manufaa makubwa sana kwa wananchi wa kawaida ni habari njema kwamba kuongeza uwezo wa mnara kutoka tekenolojia ya 3G mpaka 4G utawafanya wananchi wa Tarime kupata huduma za mawasiliano zenye kasi na ufanisi zaidi,”alisema Mainoya.

Mainoya alitumia nafasi hiyo kuiahidi serikali kwamba kama kampuni ya mawasiliano wataendelea kuwekeza hapa nchini na kupanua wigo wa mawasiliano kwa wananchi ili kuwezaa kuchangia ipasavyo katika ufanikishaji Dira hiyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items