Loading...

Jul 18, 2019

Bunge la Marekani lapinga mauzo ya silaha kwa Saudia

Bunge la Marekani limepiga kura ya kuzuia mauzo ya silaha ya kiasi cha dola bilioni 8.1 kwa Saudi Arabia na washirika wengine, ikiwa ni hatua ya kumkaidi Donald Trump ambayo huenda ikamfanya rais huyo kutumia kura yake ya turufu kupinga hoja hio.

Wabunge hao, wengi wao wakiwa wamekasirishwa na taifa hilo la Kifalme kusiana na serikali ya Riyadh kuhusika na mauaji ya mwanahaabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi mwaka jana, waliidhinisha maazimio matatu ambayo yatazuia mauzo tata yaliyotangazwa na Trump mapema mwaka huu chini ya hatua za dharura.

Maazimio hayo ya kuzuia mauzo ya silaha tayari yameidhinishwa na Baraza la Seneti, na sasa yanakwenda katika Ikulu, ambako Trump anatarajiwa kutumia kura yake ya turufu kwa mara ya tatu tangu alipoingia madarakani.

Wakosoaji wanasema mauzo hayo ya silaha yanaweza kuchochea zaidi vita vya Yemen, ambako Saudi Arabia inaongoza muungano wa kijeshi unaoungwa mkono na Marekani katika mapambano dhidi ya waasi wa Houthi wanaounfgwa mkono na Iran.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger