Cristiano Ronaldo atamani kumuona Lukaku ndani ya Juventus


Jarida la Daily limefichua siri kwamba, Cristiano Ronaldo amebariki ujio wa Lukaku ndani ya klabu ya Juventus. Jarida hilo limeripoti kuwa Ronaldo anatamani kumuona Lukaku Juventus na anamkaribisha kwa mikono miwili.

kumbukwe, Higuaini na Ronaldo wakiwa Madrid zilizuka tetesi kuwa hawakuwa na maelewano mazuri jambo lililopelekea kuuzwa kwake.

Hata Ronaldo alipotua Juventus, Higuaini alitolewa kwa mkopo, licha ya kwamba sasa amerejea tena. Jarida la Mirror pia limeeleza kuwa maboss wa Bianconeri walipomuuliza Ronaldo kuhusu mawazo yake, Ronaldo aliwaambia Lukaku hana shida asajiliwe tu.
Mpya zaidi Nzee zaidi