https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mafuriko yasababisha maafa makubwa | Muungwana BLOG

Mafuriko yasababisha maafa makubwa

Watu 67 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko baada ya mvua kali kunyesha mfululizo mashariki na kaskazini mashariki mwa nchi ya India.

Kwa mujibu wa jarida la India Times, mamlaka zimefahamisha kwamba mvua kali zilizopelekea mafuriko zilisababisha vifo  vya watu 6 katika jimbo la Uttar Pradesh, watu 22 katika jimbo la Assam, watu 33 katika jimbo la Bihar, watu 5 katika jimbo la  Mizoram na mtu 1 katika jimbo la Meghalaya.

Mamlaka pia zilibainisha kwamba watu zaidi ya milioni 9 wameathiriwa na mafuriko hayo huku watu laki 3 walihamishiwa katika makambi ya misaada.