Watoto 900 watenganishwa na familia zao mpakani mw Marekani na Mexico

Kundi la kutetea haki za binadamu limesema jana kwamba takriban watoto 1,000 wahamiaji wametenganishwa na familia zao katika mpaka kati ya Marekani na Mexico katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, licha yaa mri ya jaji kuitaka serikali ya Rais Donald Trump kusitisha mchakato huo.

Umoja wa Uhuru wa Raia wa Marekani (ACLU) umesema mahakamani wakati ukifungua kesi katika mji wa San Diego, kwamba serikali inawashutumu wazazi kwa vitendo vidogo vya uhalifu, ili kuendelea kuwatenganisha na watoto wao katika eneo hilo la mpakani.

Mfano mmoja ni Baba aliyepokonywa mtoto wake wa mwaka mmoja, kwa kusahau kumbadilisha nepi.

Serikali ya Trump ilianza kutenganisha watoto na wazazi wao mnamo Mei mwaka jana, kama sehemu ya sera ya kutovumilia kabisa wahamiaji ambao wanavuka mpaka kinyume cha sheria.
Mpya zaidi Nzee zaidi