Albert Msando akusanya Tsh. Milioni 5, alipia deni la matibabu ya mama aliyefariki


Wakili wa kujitegemea, Albert Msando amekabidhi zaidi ya shilingi milioni tano alizozikusanya kupitia akaunti yake ya Instagram kwa ajili ya kulipia deni la matibabu ya mama aliyefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na familia yake kushindwa kumudu deni la gharama za matibabu.

Mwanzoni mwa wiki iliyopita, mtoto wa marehemu alimlilia Rais Magufuli aliyekwenda kuwatembelea majeruhi wa ajali ya moto ya Morogoro na kumuomba hela ya kulipia deni la matibabu la zaidi ya shilingi milioni tano na kutoa maiti ya mama yake ili akazikwe.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items